Kituo chake cha kwanza kilikuwa mjini Mosul, ambako iliwahi kuwa ngome ya Islamic State.
Alisali kuwaombea waathirika wa vita nchini Iraq kwenye eneo la city square, miongoni mwa mabaki ya makanisa kadhaa ambayo yalivunjwa kabisa na wanamgambo.
Baada ya Mosul, baadaye Papa Francis alielekea Qaraqosh, mji wa kale wa Kikristo ambao uliovamiwa na majeshi ya Islamic State, ambako alikutana na wanachama wa jamii za kieneo katika Kanisa la Immaculate Conception.
Papa alifanya misa ya wazi kwenye uwanja wa Franso Hariri mjini Erbil kabla ya kurejea mjini Baghdad.
Kwasababu ya masharti ya Covid 19, mahudhurio ya ibada hiyo yalikuwa ni kwa watu elfu kumi tu.