Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 22:35

Papa Francis akamilisha ziara yake Iraki


Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais wa Iraki Barham Salih, alipojupuika na viongozi wengine kumuaga mgeni wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad, Iraki March 8, 2021. Picha kwa hisani ya Vatican Media/Handout via REUTERS
Papa Francis akiwa na mwenyeji wake Rais wa Iraki Barham Salih, alipojupuika na viongozi wengine kumuaga mgeni wake uwanja wa ndege wa kimataifa wa Baghdad, Iraki March 8, 2021. Picha kwa hisani ya Vatican Media/Handout via REUTERS

Mkuu wa Kanisa Katoliki ulimwenguni Papa Francis mapema Jumatatu amekamilisha ziara ya siku nne nchini Iraq ikijumuisha mikutano na viongozi wa Kiislamu na Kikristo na kuhimiza umuhimu wa kuishi pamoja kwa amani.

Rais wa Iraq Barham Salih alikuwa miongoni mwa watu mashuhuri waliokuwa kwenye uwanja wa ndege wa Baghdad kumsindikiza Francis.

Jumapili kiongozi huyo aliitembelea Mosul ambao ni mji uliyokuwa ngome ya Islamic State wakati mmoja, aliwaombea waathirika wa vita kwenye eneo la bustani.

Baadaye aliutembelea mji wa Qaraqosh wenye wakristo wengi na ambao ulichukuliwa na wanamgambo wa Islamic State.

Papa Francis pia ameongoza misa Jumapili kwenye uwanja wa michezo wa Franso Hariri mjini Ibril ambako kutokana na hali ya janga la virusi vya corona, ni watu 10,000 pekee waliyoruhusiwa kuhudhuria.

Jumamosi , kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 84 alikutana na kiyongozi wa kiislamu Ayatollah Ali la Sistani mwenye umri wa miaka 90 nyumbani kwake mjini Najaf.



XS
SM
MD
LG