Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 29, 2024 Local time: 04:24

33 wauawa kufuatia mlipuko kwenye mgodi nchini Iran


Picha inayoonyesha hali ilivyokuwa kufuatia mlipuko kwenye mgodi wa makaa ya mawe mjini Tabas, Iran.
Picha inayoonyesha hali ilivyokuwa kufuatia mlipuko kwenye mgodi wa makaa ya mawe mjini Tabas, Iran.

Mlipuko huo umepelekea moja ya mikasa mibaya zaidi katika sekta ya uchimbaji katika historia ya nchi hiyo, huku watu wengine wakiwa hawajulikani waliko saa kadhaa baada ya tukio hilo.

Walioshuhudia wameseam mlipuko huo ulipiga mgodi wa makaa ya mawe huko Tabas, takriban kilomita 540 kusini mashariki mwa mji mkuu, Tehran, Jumamosi usiku. Kufikia Jumapili, wachimba migodi waliokuwa wakilia walisimama kando ya magari ambayo yalileta miili ya wenzao, yote ikiwa imefunikwa na vumbi la makaa ya mawe.

Takriban watu 70 walikuwa wakifanya kazi wakati wa mlipuko huo. Televisheni ya serikali baadaye ilisema kwamba 17 waliaminika kuwa wamenaswa kwenye kina cha mita 200 chini ya handaki la mita 700.

Walakini, takwimu ziliendelea kubadilika Jumapili, kuhusu idadi ya watu waliopoteza maisha katika eneo hilo la mashambani, huku ripoti zingine zikieleza kwamba idadi ya vifo ilikuwa kubwa zaidi.

Mamlaka zililaumu mlipuko huo kutokana na uvujaji wa gesi ya methane. Gesi kama hizo ni za kawaida katika uchimbaji madini.

Forum

XS
SM
MD
LG