Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Julai 08, 2024 Local time: 10:58

Wanamgambo wauvamia mgodi DRC na kuuwa Wachina sita


Eneo la Djugu liloloko katika jimbo la Ituri, Kaskazini Mashariki mwa DRC
Eneo la Djugu liloloko katika jimbo la Ituri, Kaskazini Mashariki mwa DRC

Wanamgambo wameuvamia mgodi unaoendeshwa na Wachina huko Kaskazini Mashariki mwa DRC, na kuwaua raia sita wa China na wanajeshi wawili wa Congo, maafisa wa eneo hilo wamesema siku ya Alhamisi.

China imelaani shambulizi hilo, ambalo limefanyika siku ya Jumatano katika eneo la Djugu lililoko katika jimbo la Ituri lenye utajiri wa dhahabu.

Mtawala wa Djugu Ruphin Mapela amesema tukio tilo limefanywa na wanamgambo wa CODECO (Cooperative for the Development of the Congo). Kundi hilo limeundwa na wapiganaji kutoka kundi la kabila la Lendu, ambalo linadai kujilinda.

Raia sita wa China na wanajeshi wawili wa Congo waliokuwa wakitoa ulinzi katika mgodi waliuawa, amesema Mapela.

Mwakilishi wa shirika la Msalaba Mwekundu kwa Djugu, Dhekana Ernest, amesema wapiganaji wa CODECO waliwafuata Wachina waliokuwa wakichimbia dhahabu.

“Waliingia kwenye kambi yao, waliwaua raia sita wa China na wanajeshi watatu. Waathirika waliuawa kwa risasi,” alisema, na kuongeza kuwa maiti zilipelekwa mjini Bunia.

Msemaji wa jeshi katika mkoa huo alithibitisha idadi hiyo na kuongeza kuwa raia wa Congo na wanamgambo wapiganaji sita waliuawa.

Huko Beijing, Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema shambulizi kwa kampuni binafasi inayofadhiliwa na Wachina limesababisha vifo na kupotea kwa raia kadhaa China.

China inafanya mawasiliano ya karibu na mamlaka ya DRC katika kuwatafuta waliopotea, msemaji wa wizara Mao Ning aliuambia mkutano wa waandishi wa habari.

Jina la mgodi na kampuni havikuweza kupatikana mara moja.

Mwezi April 2024 Raia mmoja wa China na mlinzi wake waliripotiwa kufariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya Mgodi wao kushambuliwa na watu wasiojulikana waliokuwa na silaha katika kijiji cha Lwemba kilichopo katika wilaya ya Mambasa, zaidi kilometa 150 kusini mwa mji wa Bunia ulioko katika mkoa wa Ituri.

Chanzo cha habari hii ni Shirika la habari la Reuters

Forum

XS
SM
MD
LG