Shambulio hilo lilitokea katika kijiji cha Mayikengo katika eneo la Lubero.
Afisa wa Lubero Alain Kiwewa alisema idadi ya watu waliouwawa ni kati ya 20 na 30 iliripotiwa Alhamisi asubuhi. Alilishutumu kundi la waasi la Allied Democratic Forces (ADF), lenye uhusiano na Islamic State ambalo lilianza kama uasi nchini Uganda lakini limeendesha shughuli zake kutoka misitu ya mashariki mwa Congo kwa karibu miongo mitatu.
Afisa mwingine wa eneo hilo Macaire Sivikunula, alisema watu 25 waliuwawa wakiwemo wanawake sita. Pia alililaumu kundi la ADF.
Washambuliaji waliwataka wakazi kukusanyika sokoni kwa ajili ya mkutano kisha wakawashambulia kwa silaha za moto na mapanga, Sivikunula aliongeza.
Forum