Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 02:02

Wamarekani wenye asili ya Asia ni kundi linakua haraka lenye wapiga kura


Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Rais wa Marekani Joe Biden (kushoto) na Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Wamarekani wenye asili ya Asia ni kundi ambalo linakua kwa haraka sana lenye wapiga kura wanaostahiki nchini Marekani, kwa mujibu wa kituo cha utafiti cha Pew.

Hiyo inawafanya kuwa lengo muhimu kwa wagombea urais Joe Biden na Donald Trump.

Kuna zaidi ya wapiga kura milioni mbili Wamarekani wenye asili ya Asia katika uchaguzi huu wa rais kuliko ilivyokuwa wakati Joe Biden na Donald Trump waliposhindana mara kwanza miaka minne iliyopita, kwa mujibu wa Pew Research.

Ongezeko hili linawafanya kuwa na nguvu katika upigaji kura ambao huenda ukaleta tofauti kati ya Biden na Trump katika ushindani wa karibu ikiwemo katika majimbo ya Arizona, Georgia na Nevada, anasema mwanaharakati wa kura Christine Chen.

Christine Chen, Kura ya Mmarekani wa Asia Pacific anaeleza:

“Wakati kampeni zinaangalia kupata kura za ziada kwasababu uchaguzi huenda ukawa wa ushindi mwembamba, kwa kweli wanahitaji kuangalia wapiga kura wa Marekani wenye asili ya Asia. Kwasababu mwaka 2020, zaidi ya asilimia 21 ya wapiga kura wetu walikuwa ni wale waliopiga mara ya kwanza. Kwahiyo walikuwa na motisha sana.”

Kilichowahamasisha wapiga kura wa Marekani wenye asili ya Asia walikwa wakiangalia nani atakuwa rais? VOA ilikwenda na kuwauliza baadhi yao.

Samnang Khoeum, Mpiga Kura anasema: “Kwangu mimi, naangalia nguvu nzuri ya rais, kuwa na uwezo mzuri wa kufikiri, kufanya maamuzi sahihi na siyo kusubiri wafanyakazi waliokuzunguka ndiyo wafanye hivyo.”

Hangkannha DeSalvo, Mpiga Kura anasema: “Kwangu mimi, haijalishi umri. Ilimradi wanaweza kufanya kazi na wanaweza kuwasaidia raia wote kuwa katika hali njema, nafasi nzuri za ajira, fursa nzuri katika biashara, kujaribu kutulinda sisi na vita. Naamini hilo ni jambo kuu kwa kila mtu.”

Sophia Oumret, Mpiga Kura anaeleza: “Ningependa kuwaona watu vijana zaidi katika madarak kwasababu wana muda mrefu zaidi, hasa, kwa vile wana nguvu zaidi. Siyo kwamba wazee hawafai, lakini ni wakati wa kizazi kipya.”

Natalie Vu, Mpiga Kura anasema: “Kwa kweli nadhani kila mtu katika tiketi ya urais hivi leo ni vyema awe kwa kizazi kipya. Nadhani iwe hivyo.”

Wamarekani wenye asili ya Asia, wa visiwa vya Pacific na wenye asili ya Hawaii ni wapiga kura ambao wana wasi wasi wa sera za uchumi na mambo ya nje, kwa mujibu wa ukusanyaji maoni uliofanywa na Associated Press mwishoni mwa mwaka jana, kwa wastani watu watatu katika 10 walisema vipaumbele vyao ni mfumuko wa bei na uhamiaji.

Sichan Southimath, Mpiga Kura anasema: “Nadhani zaidi ni kuhusu uhamiaji kwasababu nimeona jamii nyingi za wa Asia, wengi wakirejeshwa Cambodia, kwahiyo ningependa kufahamu mengi zaidi kuhusu uhamiaji, tunachokifanya hapa ni kuwasaidia watu katika uhamiaji.”

Xavier Eang Lee, Mpiga Kura anaeleza: “Huduma za afya, masuala ya huduma za afya, uhamiaji. Ni muhimu sana kwangu mimi. Pia kama ilivyo kwa haki nyingine za kupiga kura na kuhakikisha kwamba uchaguzi haujavurugwa na kila kitu ni halali.”

Soben Pin, Mpiga Kura anasema: “Kuna masuala matatu muhimu kwangu mimi ni uhamiaji, uchumi na vita nchini Ukraine na Israel, nadhani kuna uwezekano wa kuongezeka kwa mzozo huko Mashariki ya Kati.”

Wapiga wa Marekani wenye asili ya Asia walikuwa ni sababu katika uchaguzi wa katikati ya awamu katika jimbo la Pennyslvania miaka miwili iliyopita na walitarajiwa kulenga kwenye kampeni zote mbili katika jimbo ambalo linaweza kwenda upande wowote katika upigaji kura wa rais mwezi Novemba.

Forum

XS
SM
MD
LG