Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Novemba 22, 2024 Local time: 03:01

Utani wa Biden wapokelewa vyema katika hafla ya waandishi White House


Rais Biden akishiriki chakula cha jioni White house na viongozi waliohudhuria mkutano wa uhusiano kati Marekani na Afrika uliofanyika Washington Desemba 14,2022.
Rais Biden akishiriki chakula cha jioni White house na viongozi waliohudhuria mkutano wa uhusiano kati Marekani na Afrika uliofanyika Washington Desemba 14,2022.

Utani wa Rais wa Marekani Joe Biden ulipokelewa vyema na wale waliohudhuria chakula cha jioni cha waandishi huko White House Jumamosi usiku hapa Washington DC.

Lakini mpinzani wake wa kisiasa, Donald Trump, alilikosoa tukio hilo wakati akijiweka sawa kwa duru nyingine mpya ya matukio ya kampeni na kufikika mahakamani wiki hii.

Biden alisema: “Uchaguzi wa 2024 umeshika kasi, na ndiyo, umri ni suala linalozungumziwa. Ndiyo mimi mtu mzima napambana na kijana wa miaka 6.”

Akifanya utani kuhusu yeye na mpinzani wake wa kisias katika uchaguzi wa mwaka huu kutaka kuchaguliwa tena, Rais wa Marekani Joe Biden alishangiliwa na vicheko kutoka kwa waandishi, watu mashuhuri na wanasiasa waliokusanyika katika chakula cha jioni cha kila mwaka cha wanahabari wa White House Jumamosi.

Rais wa Marekani Joe Biden akiwa White house Desemba 11, 2023. Picha na Reuters
Rais wa Marekani Joe Biden akiwa White house Desemba 11, 2023. Picha na Reuters

Hasa kilichojitokea, kwa mara ya kwanza, kamanda mkuu wa majeshi pia alizungumzia changamoto za kisheria za Donald Trump.

Joe Biden, Rais wa Marekani, alieleza kuwa: “Nimekuwa na wakati mzuri tangu hotuba ya Hali ya Kitaifa. Lakini Donald amekuwa na siku ngumu hivi karibuni. Unaweza kusema zenye dhoruba. Mambo hayo.”

Biden alikuwa akizungumzia kuendelea kwa kesi inayohusu kumlipa fedha mtu ili kumnyamazisha huko New York, ambapo Trump anakabiliwa na makosa 34 y auhalifu kwa kugushi rekodi za biashara. Wachambuzi wanasema hawadhani kuwa utani wa Jumamosi unaashiria mabadiliko katika mkakati wa kampeni ya Biden.

Erik Nisbet, Chuo Kikuu cha Northwestern alisema: “Alifanya hivyo kwa lugha nyepesi yenye utani, ambapo nadhani pengine hatafanya hivyo tena. Trump alitoa shutuma kuwa hili lilichochewa na Biden huko White House kumuondoa hasimu wake wa kisiasa. Hataki kjuendeleza maelezo hayo.”

Mapema Jumapili, Trump alipima kile kilichoendelea katika chakula cha jioni cha waandishi wa White House. Alibandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth kwamba tukio hilo lilikuwa kwa maneno yake “baya sana” na kwamba Biden alikuwa “kituko kabisa.”

Trump anajipanga kufanya kampeni zake huko Michigan na Wisconsin hapo Mei mosi. Ijumaa, alirejea utayari wake kwa mdahalo na Biden hata wiki hii, baada ya rais Mdemocrat kumueleza mtangazaji wa radio yuko wazi kwa mdahalo na mpinzani wa Republican baadaye mwaka huu.

FILE - Rais wa zamani Donald Trump
FILE - Rais wa zamani Donald Trump

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anaeleza: “Niko tayari na ninaweza. Kama anataka, nitafanya hata Jumatatu usiku, Jumanne usiku au Jumatano usiku. Sisi tutakuwa Michigan, jimbo ambalo ameliharibu kwasababu ya viwanda magari.”

Kubadili mawazo ya wapigakura kumpendelea mmoja wa wagombea, muda wa mdahalo utakuwa ni muhimu, anasema Profesa Erik Nisbet.

ENisbet alielezea zaidi: “Kihistoria nchini Marekani, umma kwa kawaida hata hawasikilizi au kutizama kitu gani kinaendelea katika uchaguzi mpaka mwezi Septemba, baada ya vyama kuthibitisha uteuzi wao wakati wa majira ya joto.”

Kilicho cha uhakika katika muda mfupi, ni kwamba Trump atahitaji kuzunguka kuonekana katika kampeni huku akikabiliwa na kesi huko Manhattan, ambayo inatarajiwa kuanza Jumanne.

Biden atahitaji kuendelea kutafuta uwiano sahihi kati ya kufanya kuzunguka kufanya kampeni na kutimiza majukumu yake kama rais.

Baadhi ya taarifa katika habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari.

Forum

XS
SM
MD
LG