Rais Uhuru Kenyata ameongoza maadhimisho ya sikukuu hii.
Wakati huohuo Rais wa Malawi Lazarus Chakwera yuko nchini Kenya na anahudhuria tukio hilo.
Katika sherehe hizi kwa kawaida Wakenya wanawakumbuka mashujaa waliopigana vita vya uhuru kumng’oa mkoloni Mwingereza.
Lakini maadhimisho yameongezwa na kutambua watu walio na mchango mkubwa katika nchi kwenye sekta mbalimbali ikiwemo michezo, dawa, elimu mingoni mwa nyinginezo.
Hii ni mara ya kwanza katika historia kwamba sherehe zinafanyika katika kaunti ya Kirinyaga.