Umoja wa mataifa unasema kwamba Zaidi ya watoto 465,000 chini ya miaka mitano, na zaidi ya wanawake 93,000 wajawazito na wanaonyonyesha wana utapiamlo, katika mkoa wa kaskazini mwa Kenya.
Bei ya chakula inapanda. Katika kaunti ya Marsabit ni asilimia 16 juu ya wastani takwimu zinaonyesha kutoka mamlaka ya kitaifa ya usimamizi wa majanga ya ukame (NDMA). Mbuzi haziwezi kuuzwa, ngombe pia wapo katika hali mbaya hawawezi kuuzwa na watoto wetu wanakufa na njaa, alisema Moses Loloju, mfugaji kutoka kaunti ya Isiolo ambaye alijitolea kusaidia kusambaza misaada ya chakula kutoka kwa serikali ya kaunti.
Huu ni msimu wa pili mfululizo ambapo mvua zimeshindwa kunyesha huko kaskazini mwa Kenya sehemu yenye ukame nchini humo, tofauti na kusini yenye rutuba na kijani kibichi.
Ukosefu wa mvua ina maanisha watu milioni 2.4 katika eneo hilo, watahangaika kupata chakula cha kutosha kufikia Novemba, shirika la chakula la Umoja wa Mataifa linasema.