Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 00:28

Barafu adimu barani Afrika zitatoweka katika miongo miwili ijayo shirika la hali ya hewa duniani laonya.


Nyumba zilizoko karibu na Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania katika wilaya ya Hai Dec. 10, 2009.
Nyumba zilizoko karibu na Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania katika wilaya ya Hai Dec. 10, 2009.

Barafu adimu barani Afrika zitatoweka katika miongo miwili ijayo kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa, ripoti mpya ilionya.

Barafu adimu barani Afrika zitatoweka katika miongo miwili ijayo kwa sababu ya mabadiliko ya hali ya hewa, ripoti mpya ilionya Jumanne wakati wa utabiri mkubwa wa maumivu kwa bara ambalo nchi zake zinachangia kwa kiwango cha chini kuongezeka kwa joto la ulimwengu lakini ndio zitaumia zaidi.

Ripoti hiyo kutoka Shirika la Hali ya Hewa Duniani na mashirika mengine, iliyotolewa kabla ya mkutano wa hali ya hewa wa Umoja wa Mataifa huko Scotland ambao utaanza Oktoba 31, ni ukumbusho mbaya kwamba watu bilioni 1.3 wa Afrika wanabaki hatarini sana wakati bara linapata joto zaidi, na kwa kiwango cha kasi zaidi kuliko wastani wa ulimwengu. Na wakati bado nchi 54 za Afrika zinawajibika kwa chini ya asilimia 4 ya uzalishaji wa gesi chafu duniani.

Ripoti hiyo mpya inamulika katika kupungua kwa barafu za Mlima Kilimanjaro, Mlima Kenya na Milima ya Rwenzori nchini Uganda kama ishara ya mabadiliko ya haraka na yaliyoenea yanayokuja.

Viwango vyao vya sasa vya kupungua ni vya juu kuliko wastani wa ulimwengu. Na ikiwa hii itaendelea, itasababisha kupungua kabisa katika miaka ya 2040, inasema ripooti hiyo.

XS
SM
MD
LG