Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:50

Mume wa Agnes Tirop akamatwa na kuhojiwa na polisi Kenya


Agnes Tirop, raia wa Kenya na mwanariadha wa kimataifa katika mbio ndefu, enzi za uhai wake
Agnes Tirop, raia wa Kenya na mwanariadha wa kimataifa katika mbio ndefu, enzi za uhai wake

Polisi wanasema walimuhoji mume wa Tirop, Ibrahim Rotich, jana Alhamis wakisema alikuwa akijaribu kukimbia nchini. Afisa muandamizi David Kahinga anasema uchunguzi bado unaendelea na huwenda waendesha mashtaka wakataka habari zaidi kuweza kutayarisha kesi dhidi yake

Polisi mjini Mombasa nchini Kenya wanasema mume wa mwanariadha wa mbio ndefu Agnes Tirop aliyekutwa amekufa nyumbani kwake siku ya Jumatano wiki hii atafikishwa mahakamani baada ya kukamatwa Alhamis katika mji huo wa pwani.

Polisi wanasema walimuhoji mume wa Tirop, Ibrahim Rotich, jana Alhamis wakisema alikuwa akijaribu kukimbia nchini. Afisa muandamizi David Kahinga anasema uchunguzi bado unaendelea na huwenda waendesha mashtaka wakataka habari zaidi kuweza kutayarisha kesi dhidi yake.

Chaguo mojawapo ni kumsafirisha kurudi Eldoret ambako Tirop alipatikana amekufa siku ya Jumatano. Masuala mengine bado yanaangaliwa, lakini sheria inatuhitaji tumtoe mshukiwa ndani ya masaa 24 ya kukamatwa na tutatii alisema Kahinga ambaye ni ofisa anayesimamia kituo cha polisi cha Changamwe, mahala anaposhikiliwa mshukiwa Ibrahim Rotich.

XS
SM
MD
LG