Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 21:46

Mahakama kuu ya Kenya yasitisha utoaji wa huduma namba


Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta
Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta

Mahakama kuu nchini Kenya imesema kwamba mpango wa serikali wa kutoa kadi maalum zinazojulikana nchini humo kama Huduma namba, kwa raia wake, ni kinyume cha sheria.

Mahakama imesema kwamba mpango wa kutoa kadi hizo unakinzana na sheria ya mwaka 2019 ya kulinda taarifa muhimu kuhusu kila mtu.

Jaji Jairus Ngaah, amesema kwamba Serikali ilifanya makosa kwa kutozingatia namna ya kuweka siri taarifa za raia wake kabla ya kuzindua mpango wa kuunda Huduma namba.

“Amri inatolewa na mahakama hii kusitisha mara moja mpango wa serikali wa Novemba tarehe 18 mwaka 2020 wa kutoa kadi za huduma namba kwa msingi kwamba unavunja sheria ya mwaka 2019 ya kulinda taarifa za watu”.

Mahakama vile vile imeamurisha serikali kuthathmini namna kadi hizo zinaweza kutatiza au kuwanufaisha raia wake kabla ya utoaji wake.

Serikali imekosolewa kwa kukosa kuthathmini namna ingelinda taarifa muhimu za raia wake kwa kutoa huduma namba.

Wizara ya mambo ya ndani imeamurishwa kufuata sheria katika mradi huo.

Mradi wa huduma namba ulizinduliwa kwa lengo la kuweka Pamoja taarifa zote za kila raia katika kadi moja, kwa kile kilitajwa kama hatua ya kurahihisha huduma kwa kila raia, popote nchini Kenya.

Taasisi ya kutetea katiba nchini Kenya iliasilisha kesi mahakamani kuzuia serikali kutoa huduma namba kwa kukosa kutilia maanani sheria ya kulinda taarifa muhimu za raia wake.

Tayari mamilioni ya kadi zimetengenezwa na baadhi kuchukuliwa na raia.

XS
SM
MD
LG