Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 21:56

Wahamiaji wa Haiti walalamika walivyotendewa wakiwa Marekani


Wahamiaji raia wa Haiti waliowasili baada ya vyombo vya usalama kuwasafirisha kutoka Texas waliwasili Jumapili uwanja wa ndege huko Port-au-Prince, Sept. 19, 2021.REUTERS/Ralph Tedy Erol
Wahamiaji raia wa Haiti waliowasili baada ya vyombo vya usalama kuwasafirisha kutoka Texas waliwasili Jumapili uwanja wa ndege huko Port-au-Prince, Sept. 19, 2021.REUTERS/Ralph Tedy Erol

Wahamiaji wa Haiti waliorejeshwa Jumapili katika mji mkuu wa Haiti, Port-au-Prince, kwa kutumia ndege tatu za Marekani za shirika linaloshughulikia wahamiaji na forodha - ICE wamekosoa jinsi walivyorejeshwa na kutendewa wakati wakiwa wameshikiliwa.

“Hatukuruhusiwa tuchukue vitu vyetu. Ni kama vile tulikuwa jela, hakuna chakula, wala chochote.’ Dieudonne Cassagane ameiambia VOA.

Mwanamke mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema alikuwa akiishi vizuri nchini Chile lakini hakuwa na hati ya ukaazi halali hali iliyomsababisha kuondoka huko.

Amesema raia wa Haiti walikuwa wanahudumiwa tofauti na wahamiaji wengine, wakati walipokuwa wameshikiliwa.

Utawala wa Biden ulitangaza uamuzi wake Jumamosi wa kuwarejesha maelfu ya wahamiaji waliokuwa chini ya daraja la Del Rio huko Texas kwenye mpaka wa Marekani na Mexico.

Maafisa wamesema wahamiaji wengi waliwasili kwa wingi hatua iliyosabisha kuwa vigumu kwa walinzi wa mpakani kushughulika nao.

“Wahamiaji wanaojaribu kufanya safari katika mpaka wetu lazima wajue kwamba bado tunafuata sheria ya CDC Namba 42 na hawawezi kuruhusiwa kuingia Marekani. Wataondolewa, na watarejeshwa nchini kwao kwa lazima chini ya sheria yetu.”

Mkuu wa Marekani wa Ulinzi wa Mpakani Raul Ortiz amesema hatua hiyo ina lengo la kuzuia wahamiaji wengi kufika katika eneo hilo wakati maafisa wa usalama wa Marekani wanajaribu kudhibiti wahamiaji walio chini ya daraja hilo huko texas.

XS
SM
MD
LG