“Kulingana na manusura waliofikishwa ufukweni na wavuvi na walinzi wa pwani, wanawake ishirini na watoto wawili ni miongoni mwa waliokufa maji”, msemaji wa IOM, Safa Msehli amesema kwenye twitter.
Boti za wahamiaji wanaosafiri kuelekea Italy na maeneo ya Ulaya wakitokea Libya na Tunisia, zimeongezeka miezi ya karibuni kutokana na hali nzuri ya hewa.
Maelfu ya wahamiaji wamefanya safari hatari ya kuvuka bahari miaka iliyopita, wakikimbia mizozo na umaskini barani Afrika na mashariki ya kati.