Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:13

Marekani kufanya biashara na Afrika


Rais wa Marekani Joe Biden kwenye picha ya maktaba
Rais wa Marekani Joe Biden kwenye picha ya maktaba

Utawala wa rais wa Marekani Joe Biden umezindua program inayolenga kufanya biashara na mataifa ya kiafrika kwa jina Prosper Africa Build Together, wakati ukiomba dola milioni 80 kutoka kwa bunge ili kufaulisha mradi huo.

Baadhi ya wataalam wanasema kuwa ushirikiano wa kifedha kati ya Marekani na Afrika utaimarisha uhusiano wa bara hilo na Marekani.

Wakati akizungumza kwa njia ya kimitandao Jumatano, mratibu mkuu wa Marekani kwenye masuala ya Afrika akiwa mbele ya baraza la kitaifa la usalama, Dana Banks alisema kuwa Marekani iko tayari kufanya biashara na Afrika.

Program ya Prosper Africa inalenga kuongeza viwango vya biashara kati ya Marekani na Afrika. Hii siyo mara ya kwanza kwa Marekani kubuni mpango kama huo. Mwaka wa 2000, rais Bill Clinton alitia saini mkataba wa AGOA ambao ulitoa nafasi kwa mataifa ya kiafrika kuleta bidhaa za aina 6,500 tofauti hapa Marekani bila kulipia ushuru. Mpango huo bado unaendelea baada ya kuongezwa muda wake hadi 2025.

Kulingana na taasisi ya kiuchumi ya Brookings, Afrika kusini mwaka wa 2019 ilijipatia dola milioni 917 kutokana na mauzo ya magari na vifaa vya kilimo Marekani.

Utafiti tofauti uliyofanywa na chuo kikuu cha Afrika kusini mwaka wa 2017 unaonyesha kwamba Marekani iliagiza asilimia 10 ya mvinyo wake kutoka Afrika kusini kwa gharama ya dola milioni 59.

Sasa hivi Marekani iko kwenye mazungumzo ya kibiashara na Kenya, wakati Banks akisema kuwa Marekani ina ari ya kushiriki kwenye ukuaji wa kiuchumi wa Afrika.

//Banks Act 2//

Kupenya kwa Afrika kwenye soko la kimataifa pamoja na utamaduni ulioibuka wa kibiashara vinatoa nafasi kwetu ya kuimarisha uhusiano wetu ili kuimarisha uchumi pamoja na kutoa nafasi za ajira kwa watu barani humo.//

Gerrishon Ikiara, ni mhadhiri wa masuala ya kiuchumi kutoka chuo kikuu cha Nairobi na anasema kuwa mpango huo utaimarisha uhusiano kati ya Marekani na Afrika.

Anasema kuwa lengo la Marekani ni kuimarisha uhusiano wa kiuchumi pamoja na kisiasa kwa kutumia umaarufu wake wa kimataifa. Anasema pia Marekani katika siku za karibuni imetambua bidhaa kutoka Afrika kutokana na wahamiaji wengi kutoka barani humo wanaofanya kazi Marekani.

Hata hivyo baadhi ya wakosoaji wanasema kwamba hatua hiyo huenda ijahujumu soko huro kati ya mataifa ya kiafrika ambalo lilibuniwa mwaka wa 2019 kwa lengo la kuruhusu usafirishaji huru wa bidhaa na watu kati ya mataifa.

XS
SM
MD
LG