Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:41

Ufaransa na Uingereza zakosoana kuhusu wahamiaji


FILE -Waziri Mkuu wa UIngereza Boris Johnson (Kulia) na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (Stefan Rousseau/Pool via Reuters)
FILE -Waziri Mkuu wa UIngereza Boris Johnson (Kulia) na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (Stefan Rousseau/Pool via Reuters)

Serikali ya Ufaransa imesema imemwambia Waziri wa Mambo ya Ndani wa Uingereza Priti Patel hatoalikwa tena kwenye mazungumzo ya Umoja wa Ulaya kuhusu mzozo wa uhamiaji.

Hii imekuja baada ya Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kuikosoa Ufaransa jinsi inavyokabiliana na suala hilo la wahamiaji

Ufaransa imeelezea msimamo wake huo kufuatia barua aliyoituma Waziri Mkuu Johnson Alhamisi kwa Rais Emmanuel Macron, baada ya wahamiaji 27 kufariki wakijaribu kuvuka njia ndogo ya bahari kutoka Ufaransa kuelekea Uingereza.

Macron akiwa ziarani Rome amewaambia waandishi habari barua ya Johnson ambayo ilichapishwa na kiongozi huyo wa Uingereza kwenye mtandao wa Twitter “sio njia ya busara kwa viongozi kuwasiliana juu ya namna ya kushughulikia mzozo huo wa wahamiaji”.

Uamuzi huo wa Ufaransa unabaini uhusiano mbaya kati ya nchi hizo mbili baada ya Uingereza kuondoka kwenye Umoja wa Ulaya, na changamoto ambazo watakabiliana nazo kushirikiana pamoja kwa kukabiliana na ongezeko la wahamiaji.

Chanzo cha habari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG