Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 18:58

Boris Johnson alelekea Marekani kwa mkutano wa UN


FILE - Britain's Prime Minister Boris Johnson holds a news conference on a winter COVID-19 plan in the Downing Street Briefing Room in London, Sept. 14, 2021.
FILE - Britain's Prime Minister Boris Johnson holds a news conference on a winter COVID-19 plan in the Downing Street Briefing Room in London, Sept. 14, 2021.

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson Jumapili ameondoka nchini humo akielekea Marekani kuhudhuria mkutano wa baraza kuu la Umoja wa Mataifa.

Kiongozi huyo aliandamana na maafisa waandamizi wa serikali yake kuwasihi viongozi wa dunia wanaoshiriki mkutano wa baraza kuu la Umoja wa mataifa, kuchukua hatua za haraka dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa kabla ya mkutano kuhusu hali ya hewa, COP26 utakaofanyika mwezi ujao huko Scotland.

Johnson atakuwa mwenyeji mwenza wa mkutano kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Antonio Guterres Jumatatu. Wawili hao watajadili umuhimu wa kuzisaidia nchi zinazoendelea kupunguza athari za mabadiliko ya hali ya hewa.

“Wiki hii, viongozi wa dunia watawasili New York kwenye tukio kubwa la kidiplomasia la mwaka, nitawashinikiza kuchukua hatua madhubuti kuhusu makaa ya mawe, hali ya hewa, magari, miti ili tupate mafanikio kwenye mkutano wa COP 26 na kufikia malengo yetu ya hali ya hewa”, Johnson amesema katika taarifa.

Uingereza itakuwa mwenyeji wa mkutano kuhusu hali ya hewa, COP 26 kuanzia tarehe 31 Oktoba hadi tarehe 12 Novemba mjini Glasgow. Mkutano huo unachukuliwa kama wakati muhimu sana kuzishawishi serikali, viwanda na wawekezaji kutangaza nia za dhati kwa kupunguza uzalishaji wa gesi chafu, na kupiga hatua kwa kupunguza joto duniani hadi chini ya nyuzi joto 1.5 Celsius.

Serikali ya Uingereza inasema viongozi 100 wa dunia wamethibitisha watashiriki mkutano huo.

XS
SM
MD
LG