Msafara huo ulisimamishwa na waandamanaji waliokuwa wanaupinga utawala wa zamani wa kikoloni katika jukumu lake kwenye mzozo wa kikanda na wanamgambo wa Kiislamu.
Ghadhabu zinaongezeka katika taifa hilo la Afrika Magharibi juu ya kutokuwa na uwezo kwa majeshi ya ndani na ya kimataifa kusitisha mashambulizi yanayofanywa na wanajihadi.
Majeshi ya usalama yamepata hasara kubwa sana kuwahi kutokea kwa miaka kadhaa, wiki iliyopita wakati watu waliokuwa na silaha walipowaua maafisa 49 wa jeshi la polisi na raia wanne.
Mamia ya watu waliandamana kwenye barabara ya mji wa Kaya siku ya Ijumaa kuzuia magari ya kivita ya Ufaransa kupita, mwandishi wa Roita aliyekuwepo kwenye eneo amesema.
Muandamanaji mmoja alikuwa amebaba bango lenye kusomeka “Kaya inasema kwa jeshi la Ufaransa nendeni nyumbani.”