Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 10:28

Watu 60, akiwemo meya wauawa katika shambulizi nchini Niger


Ramani inayoonyesha kijiji cha Banibangou, Niger.
Ramani inayoonyesha kijiji cha Banibangou, Niger.

Maafisa wawili wa kieneo Alhamisi waliliambia shirika la habari la Reuters kwamba takriban watu 60 akiwemo meya wa mji waliuawa kwenye shambulizi dhidi ya kijiji cha Banibangou Kusini Magharibi mwa Niger.

Afisa wa ngazi ya juu wa jimbo hilo, Zakari Karidjo, amedhibitisha kwamba meya wa mji huo aliuawa akisema kuwa hakuna kundi lililodai kuhusika kufikia sasa, kwenye eneo hilo linalopakana na Mali.

Eneo hilo lenye umaskini mkubwa na ambalo pia linapakana na Burkina Faso, katika miaka ya karibuni limeshuhudia mashambulizi kutoka wa wanamgambo, wengine wakiaminika kuwa na uhusiano na kundi la kigaidi la al Qaida.

Kando na shambulizi hilo la wiki hii makundi ya kiislamu yanaaminika kuuwa zaidi ya watu 530 mwaka huu kusini magharibi mwa Niger ikiwa idadi mara tano kulinganishwa na mwaka jana.

Mwezi Agosti makundi hayo yalifanya mashambulizi kwenye eneo la Banibangou na kuuwa watu 37 wakiwemo viongozi wa nyadhifa mbalimbali.

Makundi hayo kwa kawaida hulenga machifu, viongozi wa kidini miongoni mwa wengine wakati wa kutekeleza mashambulizi yao. Wengi wa viongozi hao wameuwawa au kutekwa nyara tangu mwanzoni mwa 2018.

XS
SM
MD
LG