Shambulizi hilo linashukiwa kufanywa na kundi la wanajihadi Jumapili, ambapo wanajeshi 49 na raia wanne wameuawa lililenga kituo cha jeshi huko Inata upande wa kaskazini.
“Hali hiyo imemsumbua kila mtu na shida hiyo lazima irekebishwe,” alisema Kabore.
Alizungumza kufuatia hasira ya umma huku kukiwa na idadi kubwa ya vifo katika mojawapo ya mashambulizi mabaya zaidi dhidi ya vikosi vya ulinzi na usalama tangu Burkina Faso ilipoanza kukabiliwa na vitisho vya wanajihadi miaka sita iliyopita.
Makamanda wawili wamefutwa kazi baada ya mamia ya vijana wadogo kwenye miji tofauti kufanya maandamano Jumanne kupinga kuongezeka hali ya ukosefu wa usalama.
Waandamanaji wametoa wito kwa rais Kabore kujiuzulu kwa kushindwa kukabiliana na hali ya kutokuwa na usalama nchini.
Lakini rais ametoa wito kwa watu kusimama Pamoja na vikosi vya usalama kutetea nch