Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 23:21

Blaise Compaore kususia kesi ya mauaji ya Sankara


Rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore
Rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore

Rais wa zamani wa Burkina Faso Blaise Compaore atasusia kesi dhidi yake inayofunguliwa wiki ijayo kuhusu mauaji ya kiongozi wa mapinduzi Thomas Sankara, mawakili wake wamesema Alhamisi.

“Rais Blaise Compaore hatohudhuria kesi ya kisiasa ambayo imepangwa dhidi yake kwenye mahakama ya kijeshi ya Ouagadougou, na sisi hatutokuwepo”, mawakili wake wa Burkina Faso na Ufaransa wamesema.

Katika kesi hiyo ambayo itafunguliwa Jumatatu, Compaore na wengine 13 wanakabiliwa na msururu wa mashtaka kutokana na kifo cha Sankara mwaka wa 1987.

Wengi nchini Burkina Faso wanatumai kwamba kesi hiyo itatoa mwanga kuhusu moja ya enzi mbaya za umwagikaji damu katika historia ndefu ya nchi hiyo yenye hali tete.

Compaore, mwenye umri wa miaka 70 alikanusha kila mara tuhuma kwamba aliamrisha mauaji ya Sankara.Sankara alichukuwa madaraka katika taifa hilo maskini la ukanda wa Sahel mwaka wa 1983, na akabadili jina la nchi mwaka uliofuata kutoka enzi ya ukoloni, Haute(Upper) Volta na kuiita Burkina Faso, ambayo inamaanisha “ardhi ya watu waaminifu”.

XS
SM
MD
LG