Shambulizi la wanamgambo dhidi ya kituo cha polisi kaskazini mwa Burkina Faso limeua maafisa 19 na raia mmoja.
Wizara ya usalama imesema kwamba shambulizi limetokea katika mji wa Inata, mkoa wa Soum, karibu na mpaka wa Burkina Faso na Mali.
Waziri wa usalama Maxime Kone, amesema kwamba huenda idadi ya waliokuwa ikaongezeka.
Shambulizi hilo ni la hivi punde katika matukio ya mashambulizi kadhaa katika nchi hiyo inayokumbwa na ukosefu wa usalama na yenye makundi kadhaa ya wapiganaji yanayohusishwa na Al-Qaida, na Islamic state.
Maelfu ya watu wameuawa na karibu mulioni 1.4 kuachwa bila makao kutokana na mashambulizi Burkina Faso.