Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:49

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la mataifa ya G7 wailaani Belarus

Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiwa na rais wa Marekani Joe Biden katika mkutano wa G7 huko Carbis Bay, Cornwall Juni 12, 2021 Leon Neal / POOL / AFP.
Waziri mkuu wa Uingereza Boris Johnson akiwa na rais wa Marekani Joe Biden katika mkutano wa G7 huko Carbis Bay, Cornwall Juni 12, 2021 Leon Neal / POOL / AFP.

Mawaziri wa mambo ya nje wa kundi la mataifa tajiri yenye uchumi mkubwa G7 walilaani Belarus kwa kupanga uhamiaji usio wa kawaida katika mipaka yake, na kutaka kusitishwa mara moja kwa kile ilichokiita "kampeni ya uchokozi na ya kinyonyaji".

Uingereza, Canada, Ufaransa, Ujerumani, Italia, Japan na Marekani zilidai kuwa utawala wa Rais Alexander Lukashenko ulipanga uhamiaji usio wa kawaida kuvuka mipaka yake.

Katika taarifa ya pamoja ambayo pia ilitiwa saini na Umoja wa Ulaya na iliyotolewa na serikali mjini London, mawaziri hao walisema: Vitendo hivi vya ukatili vinaweka maisha ya watu hatarini.

Tumeungana katika mshikamano wetu na Poland, pamoja na Lithuania na Latvia, ambazo zimelengwa na uchokozi huu wa kuchochea uhamiaji usio wa kawaida kama mbinu ya juu.

Maelfu ya wahamiaji, wengi wao kutoka Mashariki ya Kati, wamepiga kambi katika hali ya baridi kali kwenye mpaka wa Poland kwa matumaini ya kuingia Umoja wa Ulaya.

XS
SM
MD
LG