Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 21:56

Waziri Mkuu Johnson asema uhamiaji holela hautarejea Uingereza


Waziri Mkuu Boris Johnson akipiingia katika ukumbi wa mkutano wa mwaka wa Chama cha Conservative Party huko Manchester, Uingereza, Oct. 3, 2021.REUTERS/Toby Melville
Waziri Mkuu Boris Johnson akipiingia katika ukumbi wa mkutano wa mwaka wa Chama cha Conservative Party huko Manchester, Uingereza, Oct. 3, 2021.REUTERS/Toby Melville

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amesema Jumapili hatarejea katika utaratibu wa “uhamiaji holela” katika kutatua mgogoro wa mafuta, gesi na chakula cha sikukuu ya Krismas.

Johnson ameeleza kuwa hali hii ni sehemu ya matatizo ya kipindi cha mpito baada ya Uingereza kutoka Umoja wa Ulaya (Brexit).

Mwanzoni mwa mkutano na Chama chake cha Conservative, Johnson alilazimika tena kuitetea serikali yake dhidi ya malalamiko kutoka kwa wale waliokabiliwa na tatizo la kupata petroli kwa ajili ya magari yao, wafanyabiashara wa rejareja wameonya kutokea kwa uhaba wa bidhaa wakati wa Krismas, na kampuni za gesi zikihangaika na ongezeko la bei za jumla.

Kiongozi huyo wa Uingereza alitaka kutumia mkutano huo kugeuza ukurasa wa zaidi ya miezi 18 ya COVID-19 na kuangazia tena ahadi zake za uchaguzi wa 2019 kutatua ukosefu wa usawa wa kikanda, uhalifu na huduma za kijamii.

Badala yake, waziri mkuu amejikuta akirudi nyuma miezi tisa baada ya Uingereza kukamilisha kujiondoa kutoka Umoja wa Ulaya – kitu ambacho alisema kitaipa nchi uhuru wa kuboresha vizuri zaidi uchumi wake.

“Kusonga mbele kwa nchi yetu haimaanishi kuruhusu nyenzo ya uhamiaji holela, na kuruhusu idadi kubwa ya watu kufanya kazi … kile ambacho sitofanya ni kurudi katika mfumo wa zamani, ulioshindwa katika mishahara ya chini, ujuzi wa chini uliokuwa ukiendeshwa kwa uhamiaji holela,” alikiambia kipindi cha BBC cha Andrew Marr.

“Wakati watu walipopiga kura ya mabadiliko mwaka 2016 na … tena mwaka 2019 kama walivyofanya, walipiga kura kumaliza mfumo uliokuwa haufai wa uchumi wa Uingereza uliotegemea mishahara ya chini na ujuzi wa chini na uzalishaji mdogo sugu, na hivi sasa tunaondokana kabisa na hilo.”

Chanzo cha hatari hii ni shirika la habari la Reuters

XS
SM
MD
LG