Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 23:21

Waziri Mkuu wa Italia ataka nchi za G20 kutekeleza ahadi kudhibiti ongezeko la joto


Nchi za G20 zatakiwa kutekeleza ahadi zao
please wait

No media source currently available

0:00 0:00:43 0:00

Nchi za G20 zatakiwa kutekeleza ahadi zao

Waziri Mkuu wa Italia Mario Draghi ametoa wito Alhamisi kwa mataifa 20 tajiri duniani G20, kutekeleza ahadi zao za kupunguza kuongezeka kwa joto duniani kwa nyuzi joto 1.5 Celsius wakati wa mkutano wa viongozi wa kundi hilo mwezi ujao. 

Naye Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson akihutubia mkutano huo kwa njia ya mtandao amesema suluhisho litatokana na mambo manne muhimu, kuzuia utumiaji wa mkaa, kuzuia kutumia magari yanayotumia mafuta, kutoa fedha za kutekeleza mipango hiyo na kupanda miti.

Waziri Mkuu wa Italia Masrio Draghi alitoa mapendekezo yake alipokuwa anafungua Alhamisi mkutano wa siku tatu wa mawaziri wa mazingira mjini Milan ambao unawahusisha vijana wanaharakati wa kutetea kuzia mabadiliko ya hali ya hewa, ili kutayarisha agenda ya mkutano wa viongozi wa dunia wa COP26 mjini Glasgow Scotland.

Mario Draghi, Waziri Mkuu wa Italia : "Ikiwa tunataka kufanikiwa, basi nchi zote zinabidi kutekeleza jukumu lake, kuanzia mataifa ya G20. G20 ni pamoja na yale yenye kuwa na asilimia 80 ya uzalishaji jumla wa bidha duniani GDP na kutoa asili mia 70 ya gesi chafu. Wahusika wakuu na wachafuzi wote watakuwepo."

Viongozi wa G20 watakutana Oktoba 31 siku moja kabla ya kuanza kwa mkutano wa Copa 26 wakijaribu kuwa na msimamo wa pamoja kuelekea kwenye mkutano huo.

Vijana wanaohudhuria mkutano huo wamesema wanataka viongozi kuwasikiliza na kuchukua hatua za dhati na haraka. Elizabeth Wathuti kutoka Kenya ni mmoja kati ya wajumbe wanaohudhuria mkutano huo wa mawaziri.

Wathuti Anaongeza kuwa : "Kwa hivyo ujumbe wangu kwa viongozi ni kwamba ni lazima tuchukuwe hatua mara moja na kuanza kuwajibika kwa upande wa namna tutakavyo iwacha sayari hii kwa vizazi vijavyo. Kwa sababu mustakbal wetu uko hatarini, tuna wasi wasi, lakini hatuna haja ya kua katika hali hiyo ikiwa mutaanza kuchukua hatua za dharura sasa hivi.”

Kuna vijana 400 waliowasili Milan mapema wiki na walimaliza kutayarisha mapendekezo yao jana Jumatano wakitaka wahusishwe kwenye mkutano wa COP20.

Vijana hao wameeleza bayana kwamba wanataka wahusishwe pia katika utaratibu wa kuchukuliwa maamuzi juu ya jinsi ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya hali ya hewa na wanataka kuona hatua zaidi za dhati na thabiti zinachukuliwa.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akizungumza kupitia video amewashukuru vijana kwa juhudi zao zinazoleta mabadiliko katika siasa zinazohusiana na mabadiliko ya hali ya jewa.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari ikiwemo AP, AFP na Reuters.

XS
SM
MD
LG