Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 18:38

Janga la Corona linatawala katika mkutano wa mawaziri wa G20 Italy


Mfano wa chanjo dhidi ya COVID-19
Mfano wa chanjo dhidi ya COVID-19

Ushirikiano wa pande zote utakuwa muhimu katika kumaliza mgogoro huu wa afya Duniani. Blinken pia aliangazia michango ya Marekani kwa mpango wa  COVAX unaosambaza dozi za chanjo dhidi ya COVID-19 kwa nchi za kipato cha chini na cha kati na aliipongeza  Italy kuweka ajenda hii kwenye mkutano 

Janga la virusi vya Corona, mabadiliko ya hali ya hewa, na usalama wa chakula yako kwenye ajenda ya Jumanne wakati mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la mataifa ya G20 wanapokutana nchini Italy.

Mazungumzo hayo yanayofanyika katika jiji la Mareta yanawakilisha mara ya kwanza kwa mawaziri hao kukutana ana kwa ana tangu mwaka 2019. Ili kumaliza janga hilo ni lazima tupate chanjo zaidi na katika maeneo mengi waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken alisema katika hotuba yake ya ufunguzi.

COVAX msambazaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 kwa mataifa yasiyojiweza
COVAX msambazaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 kwa mataifa yasiyojiweza

Ushirikiano wa pande zote utakuwa muhimu katika kumaliza mgogoro huu wa afya Duniani. Blinken pia aliangazia michango ya Marekani kwa mpango wa COVAX unaosambaza dozi za chanjo dhidi ya COVID-19 kwa nchi za kipato cha chini na cha kati, na aliipongeza Italy kwa kufanya janga hilo kuwa lengo la mikutano ya Jumanne.

Maafisa wa wizara ya mambo ya nje Marekani walisema Blinken atasisitiza umuhimu wa kufanya kazi pamoja ili kushughulikia changamoto kama hizi za ulimwengu, kauli mbiu inayofahamika katika miezi ya karibuni wakati yeye na Rais Joe Biden waliweka njia ya sera za mambo ya nje iliyolenga sana kukuza uhusiano na washirika.

XS
SM
MD
LG