Ulaya kwa jumla ina zaidi ya nusu ya maambukizo yaliyo orodheshwa mnamo siku saba zilizopita kote duniani, ina karibu nusu ya vifo vinavyohusiana na janga hilo, hiyo ni kwa mujibu wa uchunguzi uliotolewa na shirika la Habari la ROITA.
Hicho ni kiwango cha juu cha maambukizo tangu mwezi April mwaka 2020 wakati virusi vilipoingia kwa mara ya kwanza nchini Italia.
Takriban asilimia 65 ya watu katika eneo la kiuchumi la Ulaya (EEA) ambayo ni pamoja na Umoja wa Ulaya, Iceland, Lichtensen, Norway wamepokea dozi mbili za chanjo kwa mujibu wa data lakini kasi ya utoaji imepungua katika miezi ya karibuni.
Ujerumani, Ufaransa na Uholanzi nazo zinashuhudia maambukizo hayo. Chansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema Ijumaa watu wana wajibu wa kupokea chanjo ya COVID-19 sio tu kwa ajili ya kujilinda wao lakini kuwalinda wengine pia.
“ Kwa bahati mbaya Ujerumani iko katika wimbi jingine la nne la maambukizo sasa. Tunaandikisha idadi kubwa. Watu wanaweza kuamini kwamba ni kitu cha zamani, lakini tumegundua kwamba hakijakwisha. Kwa mara nyingine tena, lazima tuhakikishe kwamba mifumo yetu ya afya haijaelemewa. Lazima tutengeneze utaratibu wa kukuza, na maana yake. “
Shirika la Afya Duniani hivi karibuni limeripoti kwamba katika wiki ya Novemba 7 imeonyesha Ulaya, ikiwemo Russia ni maeneo pekee ambayo yamerekodi ongezeko la kesi hadi asilimia 7 huku maeneo mengine maambukizi yakiwa yameshuka au yanadhibitiwa.