Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 15:04

AU yasema chanjo za Johnson & Johnson za Afrika Kusini zitasambazwa Afrika tu


Mtu anadungwa chanjo ya Johnson & Johnson katika kituo cha kuchanja, Soweto, Afrika Kusini, Ijumaa, Agosti 20, 2021.(AP Photo/Denis Farrell)
Mtu anadungwa chanjo ya Johnson & Johnson katika kituo cha kuchanja, Soweto, Afrika Kusini, Ijumaa, Agosti 20, 2021.(AP Photo/Denis Farrell)

Umoja wa Afrika umetangaza chanjo za Johnson & Johnson za COVID-19 zinazo tengenezwa Afrika Kusini hazitapelekwa tena Ulaya na badala yake zitasambazwa kati ya nchi za Afrika.

Kwa kuongezea, mamilioni ya chanjo za J&J ambazo tayari zimesafirishwa kwenda Ulaya, lakini kwa sasa zimehifadhiwa katika ghala, zitarejeshwa Afrika Kusini, mjumbe wa Umoja wa Afrika wa COVID-19 Strive Masiyiwa alisema Alhamisi.

Strive Masiyiwa
Strive Masiyiwa

Mkataba kati ya J & J na Aspen Pharmacare, kiwanda cha Afrika Kusini kinachotengeneza chanjo za J&J ambazo zilipelekwa Ulaya, kilikuwa kimepokea ukosoaji mkali kwa vile ni chini ya asilimia 3 ya idadi ya watu katika bara la Afrika wamepatiwa chanjo.

Ukosoaji huo unatokana na Idadi hiyo kulinganishwa na maeneo tajiri ya ulimwengu ambayo wameanza au wataanza kampeni ya chanjo za nyongeza.

Shirika la Afya Duniani (WHO) limetahadharisha kuwa janga hilo haliwezi kudhibitiwa mpaka pale maeneo yote ya ulimwengu yatakapopewa chanjo sawa.

XS
SM
MD
LG