Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 18:38

Chakwera aahidi kupunguza bei ya mbolea Malawi


Malawi President Lazarus Chakwera makes an acceptance speech after taking over the Southern African Development Community (SADC) Chairmanship, in Lilongwe, Malawi, on Aug. 17, 2021.
Malawi President Lazarus Chakwera makes an acceptance speech after taking over the Southern African Development Community (SADC) Chairmanship, in Lilongwe, Malawi, on Aug. 17, 2021.

Rais wa Malawi Lazarus Chakwera amesema kwamba atachukua hatua  kudhibiti ongezeko kubwa la bei ya mbolea katika mwaka mmoja uliopita.  

Kiongozi huyo amesema kuwa takriban asilimia 80 ya wakulima wa Malawi hawawezi tena kumudu bei ya mbolea.

Wakulima wa Malawi wanasema kuwa ongezeko kubwa la bei za mbolea huenda likaathiri uzalishaji chakula kwenye taifa hilo la kusini mwa Afrika ambalo hutegemea kilimo.

Bei za mbolea zimepanda maradufu wakati mfuko wa kilo 50 ukiuzwa kati ya dola 40 hadi 50 za kimarekani. Bei hizo ni karibu mara mbili zikilinganishwa na mwaka mmoja uliyopita.

Wataalamu wa kilimo wanasema kwa hali hiyo huenda ikapelekea kuongezeka kwa bei za mbolea inayotolewa kwa wakulima kupitia program maalum ya ruzuku ya serikali ,ambapo wakulima masikini hulipia dola 6 pekee kwa mfuko wa kilo 50.

Chakwera hata hivyo mwishoni mwa wiki kupitia televisheni ya kitaifa aliapa kuhakikisha kuwa bei za mbolea zinashuka. Kiongozi huo alisema kuwa ongezeko la bei ya mbolea limesababishwa na kundi la watu ambao hakuwataja majina , akisema kuwa nia yao ni kuhujumu program ya serikali ya utoaji mbolea kwa wakulima masikini.

Hata hivyo Chakwera amesema kuwa huenda bei za mbolea zitapanda kidogo ikilinganishwa na mwaka jana lakini siyo kama zilivyo kwa sasa. Shirika la watu wanaoagiza mbolea nchini Malawi hata hivyo limetetea bei za mbolea zilizoko.

Wakati shirika hilo likiwasilisha hoja zake mbele ya bunge Jumatano iliyopita, lilisema kuwa bei zilizoko zinategemea soko la kimataifa.

XS
SM
MD
LG