Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 11:13

Sierra Leonne yatarajiwa kufuta adhabu ya kifo


Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio akihutyubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York
Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio akihutyubia baraza kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York

Sierra Leone inatarajiwa kuwa nchi ya 23 katika bara la Afrika kufuta adhabu ya kifo

Sierra Leone inatarajiwa kuwa nchi ya 23 katika bara la Afrika kufuta adhabu ya kifo.

Wabunge katika taifa hilo la Afrika Magharibi walipiga kura kwa kauli moja siku ya Ijumaa kupiga marufuku adhabu ya kifo na kuibadilisha na kifungo cha maisha au kifungo cha chini cha miaka 30 kwa uhalifu kama mauaji au uhaini na kuwapa majaji nafasi ya kutumia busara zaidi wakati wa kutoa hukumu.

Sierra Leone haijaua mtu yeyote tangu 1998, wakati wanajeshi 24 waliuawa na kikosi cha risasi kwa kushiriki jaribio la mapinduzi mwaka uliotangulia. Wakati huo nchi hiyo ilikuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyomwaga damu tangu 1991 hadi 2002. Lakini zaidi ya watu 80 wamehukumiwa kunyongwa tangu wakati huo.

Rais Julius Maada Bio anatarajiwa kutia saini muswaada huo kuwa sheria.

Nchi zaidi za Afrika zimefutilia mbali adhabu ya kifo, ambayo vikundi vya haki za binadamu vinachukulia kama mabaki kikatili ya karne za utawala wa kikoloni. Mahakama kuu ya Malawi iliamua kitendo hicho kuwa kinyume cha katiba mnamo Aprili, wakati Chad ilipiga marufuku mnamo 2020.

XS
SM
MD
LG