Maadhimisho hayo ya siku ya Bastille yamefanyika kwa mara ya kwanza tangu janga la COVID-19 kuanza.
Macron alipanda gari la kijeshi, na kupungia mikono umma uliokuwa ukiangalia gwaride kutoka pembeni mwa mtaa wa Champs Elysee jijini Paris mwanzoni mwa sherehe hizo.
Mwaka huu kumeshuhudiwa kurejeshwa kwa gwaride la kijeshi baada ya sherehe za mwaka 2020 kuahirishwa na kufanyika kwa tukio la watu wachache kutokana na COVID-19.
Ilikuwa ni mara ya kwanza toka kumalizika kwa kwa vita vya pili vya dunia kwa Ufaransa kutofanya gwaride la kijeshi.
Maadhimisho hayo yanatoa heshima kwa vikosi vilivyo shiriki katika oparesheni iliyoongozwa na Ufaransa ya Takuba, ambayo wanajeshi maalumu kutoka mataifa nane ya Ulaya wanashiriki huko Mali.
Washiriki 5,000 walitarajiwa kushiriki katika maadhimisho ya mwaka 2021.