Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 01:28

Watengenezaji wa Moderna washindwa kuzipa nchi maskini chanjo ya Covid 19


Maafsa wakipokea chanjo za Moderna katika uwanja wa ndege wa Nairobi, Kenya, Sept. 6, 2021.
Maafsa wakipokea chanjo za Moderna katika uwanja wa ndege wa Nairobi, Kenya, Sept. 6, 2021.

Ripoti katika gazeti la New York Times inasema kwamba watengenezaji wa chanjo ya Moderna wamekuwa wakitoa chanjo zao kwa mataifa tajiri tu.

Ripoti katika gazeti la New York Times inasema kwamba watengenezaji wa chanjo ya Moderna ya virusi vya corona ambayo inaonekana kuwa kinga bora zaidi ulimwenguni dhidi ya COVID-19, wamekuwa wakitoa chanjo zao kwa mataifa tajiri tu, ikizifanya nchi masikini kusubiri na kupata faida ya mabilioni .

Gazeti hilo lilisema ripoti yao inatokana na habari ya Airfinity, kampuni ya data inayofuatilia usafirishaji wa chanjo.

Kulingana na maelezo ya Times, Moderna imesafirisha takriban chanjo milioni moja kwa nchi maskini. Ukilinganisha na Pfizer ambayo imesafirisha chanjo milioni 8.4 na Johnson na Johnson wamesafirisha

kiasi cha chanjo milioni 25 kwa nchi zenye kipato cha chini.

Wakati huo huo, Times imesema maafisa wa serikali katika baadhi ya nchi za kipato cha kati wameripoti kwamba nchi zao zimelazimika kulipa zaidi kwa chanjo za Moderna kuliko Marekani na Umoja wa Ulaya.

Na wakati huo huo, maelfu ya waandamanaji waliingia katika barabara za Roma Jumamosi kupinga hati mpya ya chanjo "Green Pass" ya Italia ambayo ni ya lazima kwa maeneo ya kazi ya umma na ya binafsi, kuanzia Oktoba 15.

XS
SM
MD
LG