Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa na kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo takriban wapiga kura milioni 40 tayari wamesha jiandikisha kupiga.
Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 2001 alitangaza mwaka huu kuachia madaraka.
Lakini siku chake zilizopita kumeshuhudiwa ghasia kufuatia uamuzi kwa kuwanyima karibu watu milioni 1.3 haki ya kupiga kura.
Upigaji kura ulianza majira ya saa kumi ya alfajiri na utaendelea hadi saa kumi na moja jioni.
Wachambuzi wa siasa wanasema kuwa uchaguzi huu unatazamiwa utaleta mabadilishano ya kwanza ya madaraka kwa njia ya kidemokrasia tangu nchi hiyo ipate uhuru mwaka 1960.
Kabila, ambaye amekuwa madarakani tangu kuuawa kwa baba yake 2001, ataachia ngazi katika hatua ya kihistoria.
DRC imeshuhudia utawala wa kiimla, mapinduzi ya kijeshi na vita vya wenyewe kwa wenyewe tangu lilipopata uhuru kutoka Ubelgiji mwaka 1960.