Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 10:02

DRC : Waandamanaji wavamia kituo chenye wagonjwa wa Ebola


Ramani inayo onyesha miji ya DRC ya Beni, Butembo na Yunbi ambako kuna mlipuko wa Ebola na machafuko
Ramani inayo onyesha miji ya DRC ya Beni, Butembo na Yunbi ambako kuna mlipuko wa Ebola na machafuko

Waandamanaji katika mji wa Beni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) walivamia kituo cha wagonjwa wa Ebola Alhamisi na inaripotiwa huenda wagonjwa wamekimbia, afisa mmoja wa kituo hicho Aruna Abedi ameiambia Reuters.

Maandamano hayo yametokana na maamuzi ya tume huru ya uchaguzi (CENI) ya nchi hiyo Jumatano kuamua kuitenga miji ya Beni, Butembo na miji inayo izunguka kutoshiriki katika upigaji kura katika uchaguzi mkuu wa rais uliopangwa kufanyika Jumapili kutokana na mlipuko wa Ebola na mapigano ya wanamgambo.

Mamia ya watu waliingia barabarani huko Beni mashariki ya DRC kupinga kuahirishwa kwa uchaguzi huo kutokana na hatari ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola, hatua iliyotangazwa na kamati ya taifa inayo simamia uchaguzi katika eneo hilo.

Waandamanaji hao pia walishambulia ofisi ya serikali inayoratibu mapambano na ugonjwa wa Ebola huko Beni kabla ya walinda amani kuwazuia Abedi alisema.

Wachambuzi wanasema kuwa hatua hiyo imeleta mkanganyiko mkubwa kwa wapiga kura wa maeneo hayo, wakiwa njia panda wakitafakari ni vipi uchaguzi huo utaweza kuwashirikisha wananchi wote.

Uchaguzi huo pindi utakapofanyika utahitimisha uongozi wa Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa akiendesha nchi yenye utajiri mkubwa wa madini kwa takriban miaka 18 ya misukosuko.

XS
SM
MD
LG