Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:58

UN inamatumaini uchaguzi huru utafanyika DRC


Rais Joseph Kabila
Rais Joseph Kabila

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa (UN) limeeleza matumaini juu ya kufanyika uchaguzi huru nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Disemba 30, baada ya kucheleweshwa kwa kipindi cha wiki moja zaidi.

Wapiga kura nchini DRC, wanatarajiwa kuchagua rais, wabunge na viongozi wa mikoa, Jumapili wiki hii, katika nchi hiyo ambayo imekumbwa na migogoro kwa miaka miwili chini ya utawala wa Rais Joseph Kabila.

Tume huru ya taifa ya uchaguzi CENI, iliahirisha uchaguzi baada ya ghala la vifaa vya kupigia kura kuchomwa moto.

Baraza la Usalama katika tamko lake Jumanne limeeleza matumaini yake kuwa hatua ya kuahirisha uchaguzi kwa mda wa siku 7 zaidi, itasaidia kuweka mazingira stahili kwa raia wa Congo kushiriki shughuli ya kupiga kura, uliokuwa huru na haki.

UN pia inataka wahusika katika shughuli hiyo kushiriki kikamilifu na kwa amani katika uchaguzi huo ili kuhakikisha mabadiliko kwa njia ya amani, na kwa kuzingatia katiba ya Congo na makubaliano ya Disemba 30, 2016.

Katika taarifa ya maandishi, Baraza la Usalama la umoja limesisitiza kwamba majeshi ya kulinda amani – MONUSCO na wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wapo tayari kutoa msaada utakaohitajika.

XS
SM
MD
LG