Tshisekedi alipowasili Jumanne amesema kwamba kulingana na tafiti iliyofanywa na taasisi moja ya Marekani yeye na mwenzake Kamerhe wataweza kupata karibu asili mia 50 za kura wakati wa uchaguzi wa Disemba 23.
Kiongozi huyo anasema uchaguzi ni lazima ufanyika kwa kutumia au kutotumia kompyuta zinazozusha malalamiko makubwa nchini humo kwa madai kwamba serikali inaweza kuzitumia mashine kuiba kura.
Kuna wagombea 21 wanaoshiriki katika uchaguzi huo wa rais ambapo Tshisekedi na Martin Fayulu ni wagombwa wakuu wa upinzani dhidi ya mgombea wa munagno wa vyama vya utawala Emmanuel Ramzani Shadary.