Kwa mujibu wa vigezo vya WHO, suala la dharura ya kiafya kimataifa linakadiriwa kutokana na hali isiyo kuwa ya kawaida wakati ugonjwa unapo weza kusambaa kupita mipaka na kufanya mataifa yakabiliane na hali hiyo.
Lakini Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema taasisi hiyo inakabiliana na hali ya Kongo kwa umakini mkubwa.
“Hatuta vuta pumzi mpaka pale mlipuko huu unamalizika,” amesema, akieleza matumaini yake kuwa hatua zilizo chukuliwa na WHO kudhibiti mlipuko huo zitazuia kuenea kwake ifikapo mwisho wa mwaka 2018.
Ripoti inaeleza kuwa watu 139 wamekufa na wengine 181 wamethibitishwa kuathiriwa na ugonjwa huo DRC tangu kutangazwa kwa mlipuko wa hivi karibuni wa Ebola mwezi Agosti.
WHO inasema kuwa nchi zinazopakana na Rwanda na Uganda ziko tayari kukabiliana na kuenea kwa mlipuko huu.