Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 08:51

Kabila hatagombea nafasi ya urais DRC 2018


Rais Joseph Kabila
Rais Joseph Kabila

Ramazani Shadari, Katibu Mtendaji wa chama kilichopo madarakani Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC) Jumatano ameteuliwa kuwa mgombea kiti cha urais kwenye uchaguzi wa Disemba 23, 2018.

Shadary anagombea nafasi hiyo kwa tiketi ya muungano wa vyama vinavyo tawala (FCC) nchini DRC.

Uteuzi huo umeondoa kitendawili kilichokuwepo kwamba huenda Rais Joseph Kabila ambaye amekuwa madarakani tangu 2001, angewania muhula mwengine.

Mgombea huyo wa chama hicho kilichoko madarakani ameteuliwa wakati leo ni siku ya mwisho kwa wagombea wote kuwasilisha fomu zao za maombi ya kuingia katika kinyang'anyiro hicho kwa tume ya uchaguzi ya taifa.

XS
SM
MD
LG