Maelfu ya watu wakiwemo wanawake, machifu na vijana walikusanyika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jubba Jumatatu kumpokea rais Salva Kiir akitpokea Khartoum baada ya kusaini makubaliano ya kushirikiana madaraka na makundi ya waasi na upinzani.
Siku ya Jumapili Kiir, kiongozi wa waasi Riek Machar na wawakilishi wengine wa makundi ya upinzani walisaini makubalaino mbele ya ma rais wa Sudan Omar al-Bashir, wa Ugandan Yoweri Museveni, wa Kenya Uhuru Kenyatta na wa Djibouti rais Ismail Oma Ghuelleh.
Makubaliano hayo yatamrudisha Machar kama makamu rais wa kwanza kati ya watano katika serikali ya mpito ya umoja wa kitaifa.
Katika uwanja huo wa ndege watu wengi walibeba mabango wakimsifu Kiir kama shujaa wa amani huku wengine wakipeperusha kwa fahari bendera ya Sudan Kusini . Jamii ya Wajurchol na nyinginezo walicheza ngoma za kitamaduni kwenye uwanja huo wa ndege.