Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 12:23

Marekani yapitisha sheria inayo iwajibisha DRC


Rais wa DRC Joseph Kabila
Rais wa DRC Joseph Kabila

Sheria ya 2018 inayo iwajibisha Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuheshimu haki za binadamu na kuendeleza demokrasia imepitishwa Jumanne na Bunge la Marekani.

Sheria hiyo inaweka pia vikwazo dhidi ya serikali inayo kaidi agizo hilo.

Pia inaitaka serikali ya DRC kuwaachia wafungwa wote wa kisiasa, kuondoa vipingamizi vya uhuru wa kujielezea, vyombo vya habari, kukusanyika na kujiunga na chama chochote, kuheshimu haki ya kuandamana kwa amani na kuhakikisha vyombo vya usalama vinawajibishwa kwa vitendo vya unyanyasaji ilivyo fanya.

Mbunge wa Chama cha Demokrat Karen Bass mwenye nafasi ya juu katika chama chake akiwa ni mjumbe wa Kamati ndogo ya Mambo ya Nje ya Baraza la Wawakilishi inayoangaza Afrika, ametoa tamko baada ya kupitishwa sheria hiyo.

“DRC ina fursa ya kuwa nchi tajiri kuliko zote duniani, lakini imeathiriwa na miongo mingi ya vita na ufisadi,” amesema mbunge huyo Bass.

Wananchi wa DRC kwa muda mrefu wamekuwa wakiiomba jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua ya kukiwajibisha chama tawala kuheshimu katiba ya nchi yao.

Sheria hii inakidhi maombi yao na inapeleka ujumbe kwa ulimwengu mzima kuwa Marekani haijarudi nyuma katika ahadi yake ya kulinda haki za binadamu na kuendeleza demokrasia ulimwenguni, ameandika Bass

XS
SM
MD
LG