Katika mfululizo wetu wa makala kuhusu uchaguzi huu. Leo tunatupia jicho baadhi ya changamoto zinazokabili nchi hiyo na wananchi wake ikiwa ni masuala ya Uchumi, Ufisadi, Madini, Miundombinu na Elimu. Tuungane na Sunday Shomari kwa ripoti kamili.
Jumapili Deisemba 23 wapiga kura kote nchini DRC wataelekea katika sanduku la kupigia kura , uchaguzi ambao ni wa kihistoria kwani matokeo ya uchaguzi huo ni kwamba raia wa Congo watashuhudia kubadili kwa uongozi kutoka hatamu moja kwenda nyingine kwa njia ya kidemokrasia .
Sababu za kufutwa uchaguzi
Lakini haikuwa rahisi kwani uchaguzi huo umeahirishwa mara kadhaa kwani awali ulipangwa kufanyika Novemba mwaka 2016, lakini ukafutwa na tume ya uchaguzi kutokana changamoto za usafiri na za kifedha.
Hatua hiyo ilisababisha ghasia za hapa na pale na watu kadhaa kuuawa kutokana na maandamano ya kupinga uamuzi huo.
Hisia za wapiga kura
Wapiga kura wanaguswa na mambo kadhaa katika uchaguzi huu. suala la uchumi ni kubwa katika nchi hiyo yenye utajiri mkubwa na ikiwa na idadi ya watu wanaokadiriwa kuwa karibu milioni 77 kwa mujibu wa benki ya dunia. Hata hivyo lakini uchumi wa nchi hiyobado unasua sua .
Muhaya Esekias ni mgombea wa upande wa vyama tawalaambaye anaona bado serikali ya congo haijachukua hatua za kutosha kuinua uchumi na kuinua maisha ya wananchi wake.
Jimbo la Katanga
Jimbo la Katanga nchini humo ni jimbo lenye utajiri mkubwa wa madini, na malalamiko ya wananchi kwa miaka mingi na katika uchaguzi huu yamekuwa kutofaidika na utajiri huo. Badala yake makampuni ya kimataifa na viongozi wachache wa congo ndio wanaofaidika na utajiri wa madini ya Katanga.Kahozi Kosha ni mwandishi wa sauti ya Amerika aliyeko Katanga.
Jinamizi la ufisadi
Pia DRC imekuwa ikigubikwa na jinamizi la ufisadi na rushwa viongozi waliopo madarakani na wapinzani wote kwa pamoja wameonyesha kutafuta njia za kupambana na adui huyo wa nchi yao lakini vita hii ya rushwa imesimama wapi wananchi wanaridhika na mapambano yaliopo?
Professor Deo Mirindi ni mgombea wa upinzani wa Lamukaanataka kuwepo na mahakama ya mafisadi.
Ripoti ya USAID
kwa mujibu wa ripoti ya USAID watoto milioni 3.5 nchini Congo walio na umri wa kuanza shule ya msingi hawaendi shule na serikali inatumia asilimia 12 ya bajeti ya nchi hiyoikielekezwa kwenye elimu. Lakini wapiga kura kwa upande wao wameweka umuhimu mkubwa kwa suala hiliwakitaka kuondolewe changamoto zote za kielimu hasa malipo duni kwa walimu.
Ignace Mupira ni mgombea wa vyama tawala kupitia chama cha AFDC anataka kuona mabadiliko katika bajeti hii ya elimu.
Wataka kujua chanzo cha fedha
Na je fedha hizi zitapatikjana wapi kwani bado kuna changamoto nyingi ya ukusanyaji wa kodi na bajeti ya nchi hiyo lakini mgombea huyu haoni kama hiyo ni changamoto kubwa .
Ukosefu wa usalama mapigano na ghasia ni moja ya mambo yaliochangia uharibifu miundo mbinu ya Congo kwa mujibu wa benki ya dunia Mgombea Muhaya Esekias anaona hiyo ni changamoto inayoweza kubadilishwa .
Uchaguzi wa DRC kivutio cha wengi
Kwa jumla uchaguzi huu wa drc 2018 unafuatiliwa kwa kiasi kikubwa na wananchi wa kada zote na ulimwengu kwa jumla na raia wa DRC wanataka mabadiliko katika haya masuala muhimu yanayogusa maisha yao ya kila siku na hali zao kwa jumla.