Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 09:48

Rais Kabila asisitiza uchaguzi DRC utafanyika Disemba 30


Rais wa DRC, Joseph Kabila
Rais wa DRC, Joseph Kabila

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, DRC, Joseph kabila amesema uchaguzi utafanyika Disemba 30 kama ilivyotangazwa na Tume huru ya uchaguzi, CENI, na kwamba hakuna sababu yeyote kwa raia nchini humo kuwa na mashaka.

Kabila alielezea pia kuahirishwa kwa uchaguzi kwenye miji ya Beni na Butembo huko mashariki mwa DRC hakuhusiani na msingi wowote wa kisiasa na kuwa uchaguzi utafanyika Jumapili.

Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa VOA mjini Kinshasa, Salehe Mwanamilongo, kiongozi huyo wa DRC pia anaelezea sababu za tume ya uchaguzi nchini humo-CENI kuahirisha uchaguzi wa awali uliokuwa ufanyike Disemba 23 mwaka huu.

please wait

No media source currently available

0:00 0:04:41 0:00

Wakati huo huo polisi mashariki mwa DRC walifyatua risasi za moto na gesi ya kutoa machozi siku ya Alhamisi kuwatawanya waandamanaji ambao walikuwa wakipinga uamuzi wa kuwaengua kushiriki upigaji kura wa Jumapili katika uchaguzi wa rais.

Ghasia zinazoendelea DRC kuelekea uchaguzi mkuu
Ghasia zinazoendelea DRC kuelekea uchaguzi mkuu

Darzeni ya waandamanaji walichoma matairi na kushambulia vituo vya Ebola mjini Beni baada ya tume ya uchaguzi nchini Cogo-CENI kusema itachelewesha upigaji kura mpaka mwezi Machi mwakani huko Beni, Butembo na maeneo yanayozunguka kwa sababu ya mlipuko wa Ebola.

Wagonjwa 24 walikimbia katika moja ya kituo cha matibabu wakati kiliposhambuliwa na waandamanaji wizara ya afya DRC ilisema. Waandamanaji pia waliandamana kwenye ofisi za tume ya uchaguzi mjini Beni kudai haki yao ya kupiga kura Jumapili pamoja na maeneo mengine ya nchi na kumtaka rais wa tume ajiuzulu.

CENI pia imeakhirisha upigaji kura katika mji wa magharibi wa Yumbi kwasababu ya ghasia za kikabila. Wanasiasa wa maeneo hayo wamekosoa hatua hiyo kama jaribio la kuingilia kati kura kumpendelea mgombea wa chama tawala.

XS
SM
MD
LG