Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Felix Tshisekedi alisema Jumatatu kwamba atahakikisha uwepo wa wanajeshi wa Uganda nchini Congo utakuwa wa muda maalum. wanajeshi hao ambao wanapigana sambamba na jeshi la Congo wanajitahidi kuwaondoa wanamgambo wa kundi la kiislamu.
Uganda na Congo zilianzisha operesheni ya pamoja mwezi huu dhidi ya “Allied Democratic Forces (ADF) kundi lenye silaha lenye uhusiano na Islamic State lakini wanatoa maelezo machache kuhusu upeo au muda wanaotarajia kuwepo huko.
"Nitahakikisha kwamba uwepo wa wanajeshi wa Uganda kwenye ardhi yetu ni kwa ajili tu ya operesheni hii" Tshisekedi alisema katika hotuba ya hali ya kitaifa ambayo pia ilielezea masuala ya uchumi na COVID-19.
Uingiliaji kati wa Uganda umezusha hali ya wasi wasi, kwa sababu mwenendo wa jeshi lake wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Congo mwaka 1998 hadi mwaka 2003 ambapo Uganda ilishutumiwa kwa kukalia maeneo na kupora rasilimali.