Wapiganaji wa waasi wakiislamu wanashukiwa kuwauwa raia wasiopungua 16 usiku wa jana kuamkia hii leo katika vijiji vitatu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wakazi wa vijiji hivyo wamesema Alhamisi.
Kundi linalofuatilia ghasia katika jimbo hilo la Kivu Security Tracker linasema kwenye ujumbe wa Twiteer kwamba Mashambulizi yanatajwa kufanywa na Wanajeshi wa Allied Democratic Forces (ADF) yalifanyika katika vijiji vya Mayele, Kalembo na Toya katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
Mratibu wa asasi za kiraia Maleki Mulala aliambia AFP kuwa idadi ya waliofariki ni kubwa kufikia 18, huku zaidi ya darzeni moja wakipotea.
Watu kumi na wanane, wakiwemo wanawake wanne waliuawa kwa kupigwa risasi, alisema, akilaumu jeshi kwa kushindwa kuwafuatilia.
Hata hivyo, msemaji wa jeshi wa eneo la Beni Captain Antony Mualushayi alisema wanajeshi wamepambana na kundi la magaidi wakiwemo wapiganaji wa ADF katika eneo hilo.
Taasisi ya Kivu Barometer inaorodhesha mauaji ya raia 944 huko Kivu Kaskazini na mkoa jirani wa Ituri tangu Mei wakati hali ya tahadhari ilipotangazwa ili kujaribu kudhibiti vurugu hizo.
Ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUSCO uliripoti muhtasari wa taarifa za mauaji mashariki mwa DRC yaliongezeka mwezi Agosti, yakiongozwa na vikundi vya waasi lakini pia vikosi vya jeshi.