Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 15:26

TRA yatakiwa kuacha kuwatishia wafanyabiashara


Vice President Samia Suluhu Hassan
Vice President Samia Suluhu Hassan

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetakiwa kutekeleza majukumu yake kwa kufuata taratibu, pia kujenga mahusiano bora na wafanyabiashara ili walipe kodi kwa uhuru na uadilifu bila vitisho.

Pia, wameonywa juu ya tabia ya baadhi ya watumishi wao ambao hujiunga vikundi na kuwatembelea wafanyabiashara wakijiita; Special Task Force; ambao kazi yake kubwa ni kuwatisha ili kulipa kodi.

Gazeti la Habari Leo nchini Tanzania limeripoti kuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameyasema hayo wakati akizungumza na viongozi wa Mkoa wa Kilimanjaro nchini humo baada ya kumpokea kwa ajili ya kuanza ziara ya siku saba ambayo atakagua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Alisema TRA haina sababu ya kujenga uadui na wafanyabiashara wa kada zote kwa kuwapa vitisho ili kuwashurutisha kulipa kodi, jambo ambalo siyo msimamo wa serikali.

Alisema pamoja na kuwa serikali inahitaji kila mfanyabiashara alipe kodi, lakini isingependa kutumika vitisho, bali kinachohitajika ni elimu kwa wafanyabiashara ili walipe kodi kama wazalendo wa kweli.

Makamu wa Rais alisema kuna vikundi hivyo vya wafanyakazi ambao hujiita vyenye kutekeleza maagizo ya serikali kwa maelekezo kutoka juu; na kwamba hakuna maelekezo kutoka viongozi wa ngazi za juu walioelekeza kushurutishwa kwa wafanyabiashara kulipa kodi.

Alisema mfumo wa vitisho utasababisha baadhi ya wafanyabiashara kufunga biashara zao jambo ambalo kwa namna moja au nyingine litainyima serikali mapato yake.

XS
SM
MD
LG