Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 06:02

Chadema wamtaka Magufuli kujibu hoja za kuporomoka uchumi Tanzania


Halima Mdee (Kulia) hivi karibuni alipofikishwa mahakamani. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (Kushoto)
Halima Mdee (Kulia) hivi karibuni alipofikishwa mahakamani. Pamoja naye ni Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe (Kushoto)

Chama cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimeitaka Serikali kujibu hoja kuhusu kuporomoka kwa uchumi katika utawala wa Rais John Magufuli badala ya kuwadanganya wananchi.

Halima Mdee ambaye ni Waziri Kivuli wa Mipango, Fedha na Uchumi ni mbunge wa Kawe (Chadema) amesema hoja zilizotolewa na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe hazijajibiwa na Msemaji wa Serikali Tanzania, Dk Hussein Abbas, badala yake anatoa takwimu za uongo.

Amebainisha hoja mbalimbali zinazohitaji majibu ya Serikali kueleza kwa nini kilimo kimeporomoka na itoe mpango mkakati wa kuinua kilimo nchini.

Pia, amehoji kushuka kwa uchumi wa benki ambazo hazitoi mikopo kwa wafanyabiashara.

"Tulichokuwa tunakizungumza juzi ndiyo hicho wamekizungumza jana watu wa taasisi ya sekta binafsi Tanzania (TPSF). Serikali imeondoa fedha zake kwenye benki za biashara na kwenda kuzifungia BOT. Huku kwenye mzunguko hakuna hela," amesema.

Hata hivyo, Mdee amesema katika bajeti ya mwaka 2017/18, Serikali inatarajia kukopa Sh7 trilioni, mkopo wa ndani ukiwa ni Sh6 trilioni na mkopo wa nje Sh1 trilioni.

"Serikali hii ambayo haizisaidii benki zake zichanue, ndiyo hiyo hiyo inategemea kukopa Sh6 trilioni kwenye benki hizo hizo," amesema Mdee.

XS
SM
MD
LG