Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:55

Baraza la Biashara Kenya laeleza madhara ya ongezeko la kodi kwenye mafuta


Ramani ya Kenya
Ramani ya Kenya

Kasi ya ukuaji wa uchumi wa Kenya mwaka huu huenda ikapata athari mwaka 2018 kwa kiasi kikubwa kutokana na asilimia 16 ya kodi la ongezeko la thamani (VAT) kwenye mafuta, baraza la biashara la nchi hiyo limesema Ijumaa, wakitaja bei kubwa za bidhaa na usafiri.

Kodi hiyo ambayo imeanza kutumika rasmi Septemba 1, ni sehemu ya juhudi za serikali kuboresha ukusanyaji mapato ili kupunguza mwanya wa nakisi ya fedha na kupata ongezeko la muda kwa mkopo kutoka Shirika la Fedha Duniani (IMF).

Mahakama Kuu siku ya Ahamisi ilimauru sitisho la muda kwa kodi iyo, lakini bei za petroli kwenye vituo vya mafuta ambavyo shirika la habari la Reuters ilivitembelea Ijumaa zilikuwa hazijashushwa.

“Tunaiomba serikali kufikiria tena njia mbadala za kufadhili matumizi ya maendeleo na ya sasa badala ya kutoza kodi kubwa kwenye bidhaa mbali mbali na tayari kuna mzigo mkubwa wa kodi,” taarifa ya Baraza la Taifa la Biashara Kenya (KNCCI) imesema.

Wizara ya Fedha haikuweza kupatikana mara moja kutoa maoni yake. Hazina inatarajia ukuaji wa uchumi kurejea tena kwenye asilimia 5.8 mwaka huu baada ya kipindi cha ukame, wasi wasi uliojitokeza kuhusu uchaguzi wa rais na kasi ya pole pole ya ufanisi katika sekta binafsi yalikata ukuaji wa uchumi mwaka jana hadi asilimia 4.9.

“Kunyanyuka karibuni kwa ukuaji wa uchumi kutakuwa na athari mbaya kutokana na hatua hii na huenda ikabadili ukuaji wowote ambao umeonekana katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita,” KNCCI imesema.

Kodi mpya ya VAT kwenye mafuta imesababisha bei ya petroli kupanda kwa asilimia 12 kwa lita. Watoa huduma za usafiri pia wamepandisha gharama zao na baadhi ya wauzaji wa petroli wamefanya mgomo kupinga dhidi ya ongezeko jipya la kodi, na kusababisha uhaba wa mafuta. Kodi awali ilihuuisha sheria iliyopitishwa mwaka 2013, lakini iliakhirishwa mara kadhaa, huku kukiwa na upinzani kuhusu matokeo yake.

Mamlaka ya mapato ilipitisha kodi hiyo Jumamosi lakini Rais Uhuru Kenyatta huenda akabadili maamuzi hayo kwa kutia mswaada wa kuiakhirisha tena.

Justin Muturu, Spika wa Bunge la Taifa, ameiambia Reuters siku ya Ijumaa kwamba bunge lilikuwa likijadiliana na wizara ya fedha kubuni njia za kulishughulikia suala hili la kodi.

Wafanyabiashara wa Kenya na watu wa kawaia kwa kawaida hulalamikia mzigo mkubwa wa kodi. Baraza la biashara limesema serikali huenda ikapanua wigo wa kodi na kuongeza viwango vya kodi kwa asilimia 50 kutoka kiwango cha sasa cha asilimia 17.

Pia imeisihi serikali kupunguza matumizi, kupunguza matumizi mabaya ya fedha za umma na kukabiliana na rushwa, ambayo tafiti zilizopita zimebaini kuwa husababisha hasara kubwa mpaka theluthi moja ya bajeti ya mwaka ya serikali.

XS
SM
MD
LG