Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:04

Wanawake wa Tanzania wachangamkia fursa za biashara Burundi


Makamu wa pili wa rais wa Burundi Joseph Butore akifungua maonesho ya kwanza ya biashara.
Makamu wa pili wa rais wa Burundi Joseph Butore akifungua maonesho ya kwanza ya biashara.

Nchini Burundi, wafanyabiashara wa nchi jirani ya Tanzania wamepata fursa ya kutangaza biashara zao nchini humo kupitia maonyesho ya kwanza kabisa ya kihistoria yalioandaliwa na nchi hizo mbili.

Wafanyabiashara wengi wao akinamama ndiyo idadi kubwa katika maonyesho haya yanayofanyika wiki hii na wameomba wawekewe mazingira mazuri ya kuwekeza nchini humo.

Tanzania ndiyo lango kubwa la kuingiza bidhaa nchini Burundi, ambapo asilimia sabinii ya bidhaa zinazoingizwa nchini Burund hupitia bandari ya Dar es Salam, lakini hadi sasa kuna tatizo la usafirishaji wa bidhaa hizo, ingawaviongozi wanadai kuwa juhudi zinafanyika ili kuondoa vipingamizi hivyo.

Mwandishi wa idhaa ya Kiswahili VOA ameripoti Alhamisi kuwa wafanyabishara kutoka Tanzania, wanatumia fursa hiyo kutangaza bidhaa zao ikiwa ni moja ya mkakati wa kupenya katika soko la Burundi.

Madhumuni yake ni kukuza na kuimarisha uhusiano wa kibiashara kati ya Tanzania na Burundi. Kiwango cha biashara kati ya Burundi na Tanzania ni milioni sabiini huku asilimia 35 ya bidhaa hizo zikiwa zinatengenezwa nchini Tanzania.

Jamila Rajabu ni mmoja wao, anasema ni kwa sababuTanzania imewawezesha akinamama.

Annick Kabatesi ni mjasiriamali wa kike nchini Burundi, anaipa changamoto serikali ya Burundi kuwawezesha Warundi ilinaowaweze kupeleka bidhaa zao kwenye soko la Tanzania.

Lakini vile vile wanachoomba ni akinamama wajasiriamali kurahisishiwa kuingiza bidhaa zao Burundi.

Mbali napicha mbaya ya Burundi kwenye ulingo wa siasa kimataifa kuhusu suala la usalama, changamoto nyingine ya kuwekeza nchini Burundi kwa wagenini usafirisishaji wa bidhaa kutoka bandari ya Dar es salam hadi Bujumbura. Dieudonnee Dukundane ni katibu mtendaji wa tasisi ya usafirishaji wa njia ya kati ama central corridor, anasemahata hivyo juhudi zinafanyika ili kuboresha hali hiyo.

Imetayarishwa na Mwandishi wetu wa Haidallah Hakizimana, Burundi

XS
SM
MD
LG