Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters mzozo nchini Sudan Kusini na ukame wa muda mrefu ambao umelikumba eneo hilo umewaacha zaidi ya watoto milioni 15 wakiwa na shida ya chakula, maji, huduma za afya, elimu au ulinzi imesema idara ya Umoja wa Mataifa ya kuhudumia watoto- UNICEF.
Nchi ya Ethiopia, Somalia na Kenya zimeshuhudia kupanda kwa viwango vya njaa miongoni mwa watoto katika wiki za karibuni huku maeneo kadhaa yakiripoti zaidi ya theluthi moja ya watoto wana matatizo ya afya ikiwa ni matokeo ya hali hiyo taarifa ya World Vision ilisema.
“Bado tuko katika hali ya hatari wakati zaidi ya watoto 800,000 wana utapiamlo uliokithiri na wako katika hatari ya kukumbwa na njaa ambayo itapelekea vifo amesema Mkurugenzi wa Afrika Mashariki wa World Vision, Christopher Hoffman. "Tuna wiki chache tu kusitisha hali hii kutokea”.