Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 21:29

Tanzania yapunguza ada ya kiingilio katika hifadhi za wanyama kwa raia wa EAC


Wilaya ya Hie, ambayo iko chini ya Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Picha ya Dec. 10, 2009.
Wilaya ya Hie, ambayo iko chini ya Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania. Picha ya Dec. 10, 2009.

Mamlaka nchini Tanzania imepunguza ada ya kiingilio katika hifadhi za wanyama kwa raia wa Afrika Mashariki ikiwa ni hatua ya kuvutia watalii zaidi kutoka nchi jirani.

Kulingana na programu ya hivi karibuni iliyotolewa na Wizara ya Maliasili na Utalii, Tanzania inalenga kupata wageni kutoka nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutembelea mbuga za wanyama, maeneo ya kihistoria, na watu wazima raia wa Afrika Mashariki sasa watalipa Tsh 10,000 ($4.2), ada ambayo itatozwa kwa watu wazima raia wa Tanzania.

Dkt Pindi Chana, Waziri wa Maliasili na Utalii , alisema serikali ya Tanzania pia itajikita katika mikutano na makongamano kupitia maonyesho, makongamano na utalii mwingine.

Lakini ni uamuzi wa ada ya kiingilio ambao ni muhimu zaidi. Wageni kutoka nchi za jirani mara nyingi walikuwa wanalalamika kutozwa ada zaidi wakati Watanzania walilipishwa kwa mujibu wa makubaliano ya EAC wanapotembelea nchi jirani.

Tanzania ilikuwa imekataa kuingia katika programu ya visa moja ya utalii ya Kenya, Uganda na Rwanda ambayo inaruhusu mgeni kutembelea nchi hizo tatu kwa kutumia visa moja iliyotolewa na mojawapo ya nchi hizo tatu.

Dkt Chana alisema kushushwa kwa ada hiyo na kutolewa kwa motisha kwa kufanya mikutano pia kutasaidia kuvutia watalii milioni tano wenye kuchangia dola bilioni 6, lengo lililowekwa kwa mwaka 2025 chini ya Mpango wa Maendeleo ya Utalii wa miaka mitano.

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.1
Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.1

Hatua ya awali ni kushirikiana na sekretarieti ya EAC huko Arusha kufikia mwaafaka juu ya makatazo na harakati za watu katika eneo la EAC chini ya Safu ya Utalii ya Afrika Mashariki (EATF).

Chini ya EATF, Tanzania inaungana na wengine katika eneo la EAC kuunda kituo kimoja cha utalii kwa raia wa eneo hilo bila ya vikwazo kuwepo katika maeneo ya kuingilia mpakani na muafaka wa ada za kuingilia katika maeneo ya utalii, hasa mbuga za wanyama na maeneo ya turathi.

Nchi hiyo pia imeanzisha visa za kieletroniki (eVisa) kwa wageni wanaoingia Tanzania.

Serikali pia inalenga kuongeza idadi ya wasafiri wa ndege kutoka milioni 2.94 hivi sasa mpaka milioni 3.09 mwakani, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imeeleza.

TAA hivi sasa inakaribisha ndege za kimataifa, ikitumia fursa ya kuongezeka kwa utalii baada ya kuzinduliwa kwa filamu ya Royal Tour documentary USA katikati ya mwezi Aprili.

Bodi ya Utalii ya Afrika imekuwa ikihimiza kwa anga zilizowazi Afrika zikienda sambasamba na mashirika ya ndege yenye ushindani mkubwa, na ubia, uwekezaji wa pamoja na aina ya ushirika mwengine.

XS
SM
MD
LG